Ingia
Ingia
Ingia
Chagua Lugha

Tafsir: Bani Israil 17:67

17:67
واذا مسكم الضر في البحر ضل من تدعون الا اياه فلما نجاكم الى البر اعرضتم وكان الانسان كفورا ٦٧
وَإِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فِى ٱلْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّآ إِيَّاهُ ۖ فَلَمَّا نَجَّىٰكُمْ إِلَى ٱلْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ ٱلْإِنسَـٰنُ كَفُورًا ٦٧
وَإِذَا
مَسَّكُمُ
ٱلضُّرُّ
فِي
ٱلۡبَحۡرِ
ضَلَّ
مَن
تَدۡعُونَ
إِلَّآ
إِيَّاهُۖ
فَلَمَّا
نَجَّىٰكُمۡ
إِلَى
ٱلۡبَرِّ
أَعۡرَضۡتُمۡۚ
وَكَانَ
ٱلۡإِنسَٰنُ
كَفُورًا
٦٧
Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo kuvueni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na mkipatikana na shida baharini mkakaribia kuzama na kuangamia, wanapotea kwenye akili zenu wale waungu ambao mlikuwa mkiwaabudu, na mkamkumbuka Mwenyezi Mungu Muweza, Peke Yake, Awasaidie na Awaokoe, hapo mnamtakasia katika kutaka msaada na uokzi, na Yeye Anawasaidia na Anawaokoa. Anapowaokoa kwa kuwaegesha kwenye nchi kavu, mnageuka mkaacha Imani, kumtakasia Mwenyezi Mungu na matendo mema. Na huu ni katika ujinga wa binadamu na ukafirir wake, kwani binadamu ni mkanushaji sana neema za Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka.